Jinsi ya kutengeneza kahawa

Karibuni mjifunze nami
Katika somo letu la Leo tutajifunza jinsi ya kutengeneza chai ya kahawa. Ambayo unaweza ukainywa ukiwa umepumzika, unajisomea au ukiwa unafanya kazi pia waweza kutumia chai ya kahawa ni nzuri Sana na inafaida kubwa kwa mwili wa binadam faida hizo za kunywa chai ya kahawa ni
  1. Kahawa huchangamsha akili yako, kama upo kazini unaweza kujikuta unasinzia au kupatwa na uchomvu, utumiaji wa chai ya kahawa husadia kuchangamsha mwili pamoja na akili yako ili kuimarisha ufanisi wa kazi, kahawa ina glucose ambayo husaidia kuongeza nguvu katika mwili
  2. Kahawa husaidia kufanya sawa msukumo wa damu katika mwili.
  3.  Kahawa husaidia mwili kujikinga na magonjwa kwa kuzipa nguvu chembe chembe za mwili zinazokinzana na magonjwa mwilini kwani kahawa huupa nguvu mwili na kuufanya upambane vyema na magonjwa na kukinga mwili dhidi ya magonjwa hasa kansa
  4. Kahawa husaidia kupunguza maumivu ya kichwa, hivyo baada ya kutumia panadol, au Headex inashauriwa utumie kiwango kikubwa cha maji au chai ya kahawa kuponya maumivu ya kichwa.
  5. Kahawa hupunguza msongo wa mawazo kwani inamiliki homini inayojulikana kama Dopamine na Seratonin ambayo inasaidia kukuchangamsha na kupunguza msongo wa mawazo kwenye ubongo wako
  6. Kahawa huongeza uwezo wa kuweka kumbukumbu ya vitu kwani kahawa hukupa nguva ya kujifunza zaidi na kukumbuka mambo kwa ufasaha zaidi.
  7. Kahawa husaidia kupunguza uzito wa mwili kwani hupunguza hamu ya kula kwa muda mfupi.   Kwa kuangalia faida hizo tujifunze sasa kutengeza kahawa bora majumbani kwetu
Mahitaji:
Sukari vijiko 3 vya chakula
Kahawa vijiko 2 vya chakula 
Maziwa robo kikombe 
Maji ya moto yaliyo chemka.

Hatua
.
-Hatua ya kwanza unachukua sukari na kahawa una weka pamoja kwenye kikombe mchanganyo wako wa kahawa na sukari.
-hatua ya Pili unachukua mchanganyo wako wa sukari na kahawa na kuweka vijiko viwili vidogo vya maji au kijiko kikubwa kimoja cha cha kula.
-hatua ya tatu Una koroga mchanganyiko wako kwa kuupiga piga Kama yai  mpaka upate tope zito unaendelea kukoroga utaona mchanganyiko wako unaanza kubadilika rangi na kua rang ya maziwa jitahidi mchanganyiko wako Ubadilika rangi baada  ya hapo
-Hatua ya mwisho unachukua maziwa yaliyochemshwa unachanganya na mchanganyiko wako wa sukari, kahawa na maji....na unapo changanya mchanganyiko wako na maziwa utaona povu likipanda kwenye kikombe chako na chai yako ya kahawa itakua tayari na yenye kua na radha au test ya chocolate.
Ni nzuri Sana na karibuni nyote kujifunza nami mambo mbali mbali.

Comments

Popular posts from this blog